
Makocha Jurgen Klopp wa Liverpool (Kulia) na Frank Lampard wa Chelsea (Kushoto) wakizungumza jambo katika moja ya mechi zilizozikutanisha timu zao.
Makocha wanaowania tuzo hiyo ni Jurgen Klopp, Frank Lampard, Brendan Rodgers n a Chris Wilder.
1-Jurgen Klopp.
Ameingia kwenye kinyanganyiro hiki baada ya kuiongoza Liverpool kutwaa ubingwa wa ligi kuu England kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30.
Katika michezo 38 ya ligi kuu chini ya klopp Liverpool imeshinda michezo 32 sare michezo 3 na wamepoteza michezo 3.
Pia msimu huu Klopp ameshinda tuzo za kocha bora wa mwezi mara 5,lakini pia wakiweka rekodi ya kushinda michezo 18 mfululizo.
2-Frank Lampard.
Amekiongoza kikosi cha Chelsea kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ukiwa ni msimu wake wa kwanza kwenye EPL na kukata Tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya UEFA Champions League msimu ujao .
Katika michezo 38 chelsea imeshinda michezo 20 sare 6 na wamefungwa michezo 12.
3-Brendan Rodger.
Amekiongoza kikosi cha Leicester city kumaliza nafasi ya 5 kwenye EPL huku wakiweka rekodi ya ushindi mkubwa msimu huu baada ya kuifunga Southampton mabao 9-0 ambao pia ndio ushindi mkubwa ugenini msimu huu.
Leicester imeshinda michezo 18 sare michezo 8 na wamefungwa michezo 12 katika michezo 38 ya EPL.
4-Chris Wilder.
Kocha wa Sheffield amekuwa kocha wa kwanza kukiongoza kikosi kilichopanda daraja kuruhusu mabao machache ambapo kikosi hicho kimeruhusu mabao 39 tu ikiwa ni rekodi kwa timu iliyopanda daraja.
Sheffield utd chini ya kocha huyo imefanikiwa kumaliza nafasi ya 9 lakini pia alifanikiwa kuvuna alama 4 dhidi ya Chelsea, Arsenal Tottenham Hotspurs na Wolves.
Katika michezo 38 kikosi cha Chris Wilder kimeshinda michezo 14 sare 12 na wamepoteza michezo 12.