
Katibu wa chama cha mpira wa magongo Tanzania THA Mnonda Magani amesema, mashindano hayo ndiyo yatakayotumika kuzipata timu zitakazoshiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika mwaka 2017.
Magani amesema, Klabu za TPDF pamoja na Magereza wanaume ndizo zitakazowakilisha Tanzania katika mashindano ya Klabu bingwa Afrika ya mwaka huu yatakayofanyika Desemba Mwaka huu nchini Zimbabwe.