Jumatano , 12th Mei , 2021

Baada ya kutangazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2020/21 kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa huu ni msimu utakao baki kwenye kumbukumbu zao kwani ulikuwa ni msimu mgumu mnoo kuliko misimu yote na amekiri kuwa EPL ndio Ligi ngumu zaidi.

Guardiola

Manchester City walitangazwa rasmi kuwa mabingwa wa EPL msimu huu, usiku wa jana mara baada ya Manchester United kufungwa na Leicester City mabao 2-1 kwenye mchezo amabao ulipigwa katika dimba la Old Traford.

Matokeo hayao yaliifanya Manchester City yenye alama 80 kuendelea kuwa na tofauti ya alama 10 dhidi ya Manchester United wanaoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na alama 70, ikiwa imesalia michezo mitatu hivyo hakuna timu inayoweza kufika alama walizonazo City.

Baada ya kuutwaa ubingwa huo ambao ni wa tatau (3) kwa Man City ndani ya mismu minne chini ya kocha huyo raia wa Hispania. Kuhusu ubingwa huu Pep amesema,

“Huu umekuwa msimu wa tofauti sana. Huu umekuwa mgumu sana, tutaukumbuka msimu huu kila wakati kwa jinsi tulivyoshinda. Ninajivunia kuwa meneja wa kikosi hiki na kundi hili la wachezaj,i ni wapekee sanaa. Tumepitia mengi msimu huu vizuizi na shida zote ambazo tumekabiliana nazo na kuonyesha mwendelezo bora hakika ni wa kushangaza tena bila kuchoka.”

Guardiola ambaye amawahi kufanya kazi nchini Hispania na Ujermani akasisitiza kuwa ligi kuu ya England ni ligi ngumu zaidi

"Nimekuwa Hiispania, nimekuwa Ujerumani na naweza kusema hii ni ligi ngumu zaidi, ningesema kwa mbali. Kwa hivyo inamaana kubwa kwa kila mtu."

Guardiola mwenye umri wa miaka 50 hili linakuwa ni taji lake la nane(8) tangu ajiunge na Manchester City mwaka 2016, lakini pia ni taji la pili msimu huu baada ya kutwaa ubingwa wa Carabao Cup.