
Kingsley ComaN - winga wa Bayern Munich
The Gunners wanahitaji mshambuliaji na wamekuwa wakihusishwa kupata huduma ya mmojawapo kati ya Viktor Gyokeres, Victor Osimhen na Benjamin Sesko ili kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji na kushinda taji la Ligi Kuu msimu ujao.
Washambuliaji wa Arsenal msimu huu wa 2024/25 wameshindwa kufikia malengo kufuatia majeraha makubwa ya Bukayo Saka, Gabriel Jesus na Kai Havertz. Pia kumekuwa na mashaka ya majeraha kwa Gabriel Martinelli na Leandro Trossard kutopatikana Uwanjani mara kwa mara.
Coman ambaye amehudumu ndani ya Bayern kwa muongo mmoja, ameibuka mjadala hivi karibuni huku Liverpool na Tottenham Hotspur wakidaiwa kuonyesha nia.
Lakini Sky Germany imeripoti kwamba Arsenal wamefanya mawasiliano na kambi ya mchezaji, wakionyesha nia yao ya kumnunua nyota huyo mwenye umri wa miaka 28.
Bayern imetajwa kuwa inaweza kumuuza Coman endapo watamsainisha Leroy Sane mkataba mpya, lakini kwa mshahara mdogo na sehemu kubwa ya nyongeza zinazohusiana na kiwango chake.