Jumatano , 7th Oct , 2020

Kinara wa mabao wa VPL, Prince Dube ameshindwa kujiunga na timu yake ya Taifa (Zimbabwe) kutokana na majeraha ya nyama za paja.

Mshambuliaji wa Azam Fc, Prince Dube(Kulia) aliposaini mkataba wa kuitumikia Azam Fc ambapo pembeni yake akiwa na Mtendaji mkuu wa wanalambalamba Abdulkarim Amin.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Azam Zacharia Thabit  imearifu kwamba Dube aliumia kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar, Jumapili usiku, ambapo alitakiwa aripoti kwenye kambi ya timu yake ya Taifa Jumanne.

Zimbabwe inajiandaa kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi, Okroba 11 jijini Blantryre nchini Malawi.

Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa, amesema hali yake siyo mbaya na amepewa mapumziko ya wiki moja kabla ya kuanza mazoezi mepesi kisha arudi katika hali yake ya zamani.

 

Nyota huyo amepachika magoli matano hadi raundi tano inakamilika huku akiwa ametoa pasi mbili za usaidizi wa magoli.