
Akizungumza hii leo jijini Dar es salaam Afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF Baraka Kizuguto amesema benchi la ufundi limefanya kazi nzuri na kikosi kimepambana kwenye mechi licha ya kukosa bahati katika changamoto ya mikwaju ya penati.
Kizuguto amesema mara baada ya kurejea kwa The Kilimanjaro Stars wachezaji watajiunga na klabu zao ambazo zinarejea tena kwenye mshikemshike wa ligi kuu ya soka Tanzania bara inayorejea hivi karibuni.
Vilevile amesema wao kama TFF wataendelea na mipango ya timu hiyo ambayo ina mechi za kimataifa kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2017 dhidi ya Chad nyumbani na yugenini mwezi March mwakani.
The kilimanjaro stars imetupwa nje ya michuano ya Chalenji na Ethiopia kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-3 baada ya mchezo huo wa robo fainali kumalizika kwa sare ya bao 1-1.