
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa barani afrika Dar Younga afrikans kesho usiku wanatupa karata yao muhimu katika mchezo wa marudiano wa michuano hiyo dhidi ya mabingwa watetezi Al Ahly mchezo utakaofanyika uwanja wa El Max mjini Alexandria huku Yanga ikiwa na faida ya goli moja ililopata katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Da es salaam wiki moja iliyopita
Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Yanga Afrika, mapambano yanaendelea
Wakati hayo yakiendelea kwa yanga wapinzani wao Simba wao kesho watakua na kibarua kizito ugenini katika ligi kuu ya soka tanzania bara kwa kuvaana na Tanzania Prisons katika uwanja wa sokoine jijini Mbeya
Ambapo mmoja wa wadau wa soka ambaye ni mwanachama wa klabu hiyo Mwina Seif Kaduguda Simba wa Yuda amesema kuwa kufanya vibaya kwa timu hiyo ni kutokana na timu hiyo kukumbatia matajiri ambao hawako kwajili ya timu bali kwa maslahi yao.