Jumapili , 27th Jun , 2021

Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa Yanga kupitisha rasimu ya mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo aligeuka kivutio kwa hotuba na simulizi zake zilizojaa mzaha na masikhara.

Rais mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete.

Mh. Kikwete aligeuka kivutio kikubwa kwenye hotuba yake pamoja na kuikumbusha klabu yake pendwa maarufu kama ‘wananchi’ kufanya usajili mzuri  kwa wachezaji wenye  hadhi  pamoja na kuvumilia makocha, lakini hakuacha kuchomekea  imani za kishirikina katika timu hiyo miaka ya nyuma.

Mkutano  huo uliofanyika katika ukumbi wa DYCC uliyopo Temeke  na kufungiliwa rasmi saa 4:00 asubuhi ,ulikuwa na ajenda kadhaa zinazolenga kuijenga upya klabu, japo ile yenye nguvu ilikuwa kubariki mchakato wa  mabadiliko ya klabu kwenda kwenye mfumo wa  uwekezaji.

Pia  wajumbe wa  mkutano mkuu walionekana kufurahishwa zaidi na uwakilishwaji  wa mpango wa ujenzi wa makazi  ya wachezaji na viwanja vya kuchezea kule Kigamboni.