
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa ufukweni
Ameongeza kuwa katika kikosi hicho walitakiwa wachezaji 13 lakini nafasi ya mlinda mlango bado ipo wazi na kocha anatarajia kumtangaza hivi karibuni.
Deo amesema, nafasi ya mlinda mlango ilikuwa ni ya Juma Kaseja lakini kutokana na kubanwa na ratiba imewabidi kuacha nafasi hiyo ili kuweza kuangalia mlinda mlango mwingine ambaye ataungana na kikosi ambacho kitaingia kambini Desemba Mosi mwaka huu.
Deo amewataja katika kikosi cha wachezaji 12 kitakachoingia kambini wachezaji watatu ni kutoka visiwani Zanzibar.
Wachezaji walioitwa kambini ni Rabi Ally Rabi, Rajab Gana, Halifa Mgaya, Loland Revocatus, Mwalimu Akida, Juma Ibrahim, Kashilu Salum, Mohamed Rajab, Twalib Ally, Ahmada Ally, Kassim Kilungo na Samuel John.