
Akizungumza jijini Dar es salaam, Rais wa Klabu ya Simba, Evance Aveva amesema katika zoezi la usajili linaloendelea, ndani ya wiki hii wanatarajia kumpokea aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Hamisi Friday Kiiza ‘Diego’ kwa ajili ya kukitumikia kikosi hicho.
Kiiza aliachwa na Yanga SC Desemba mwaka jana, baada ya kuitumikia klabu hiyo tangu mwaka 2011 ambapo aliachwa ili asajiliwe mshambuliaji Mliberia, Kpah Sherman.
Mganda huyo mkali wa mabao tangu hapo amekuwa hana timu, baada ya mpango wake wa kwenda kucheza Fanja ya Oman kushindikana Januari mwaka huu.