Alhamisi , 16th Jun , 2016

Baada ya kupata viongozi wapya wa chama cha Karate Tanzania, Baraza la Michezo nchini Tanzania BMT limekiagiza chama hicho kufanya mabadiliko ya katiba.

Mwenyekiti wa Chama cha Karate Tanzania, Willy Ringo

Baada ya kupata viongozi wapya wa chama cha cha karate Tanzania, Baraza la Michezo nchini Tanzania BMT limekiagiza chama hicho kufanya mabadiliko ya katiba.

Mwenyekiti wa karate Tanzania Willy Ringo, amesema katiba hiyo lengo lake hasa ni kuunda vyama vya Wilaya na Mikoa vya mchezo huo, ambavyo kwa sasa hakuna.

Kiongozi huyo wa karate, ambaye pia ni mkufunzi wa mchezo huo, anayetoa mafunzo kwa vijana kwenye kituo cha utamaduni wa Urusi, jijini Dar es Salaam, amesema mchakato mzima wa katiba umeshakamilika na wanataraji hivi karibuni kuitisha mkutano mkuu wa wanachama, ili kupitisha katiba, kabla ya kupelekwa kwa msajili.