Jumatano , 15th Jun , 2022

Nahodha wa Engaland Harry Kane amemkingia kifua kwa kumtetea kocha mkuu wa timu hiyo Gareth Southgate kwa kusema kocha huyo ndiye mtu sahihi wa kuinoa England na watu hawapaswi kuwa na shaka nae hata kama England kufungwa 4-0 dhidi ya Hungary.

(Nahonda Harry Kane na kocha Gareth Southgate - England)

Kikosi cha Southgate kilipokea kichapo hicho toka kwa Hungary katika uwanja wa Molineux ukiwa ndio mchezo wao wa mwisho wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya UEFA Nations league kwa mwezi huu wa sita huku mlinzi wa kati wa England John Stones alitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Southgate amekiri kuwa anapaswa kuwajibika kwa mtokeo hayo huku akiwatetea wachezaji wake. "Tulichagua timu changa yenye nguvu, lakini mchezo ulipoanza kwenda kinyume nao, ndio hali ikwaha hivyo. Na mwisho w a yote hilo ni jukumu langu." Alisema Southgate

Pia kocha huyo wa Simba watatu amewasihi mashabiki wataifa hilo waliokua na hasira kali kuendelea kua pamoja na kikosi chake kuelekea michuano ya Kombe la Dunia baadae mwaka huu, na wala wasikate tamaa.

Ushindi huo wa Hungary ulikuwa ni wa kwanza kuupata katika ardhi ya Uingereza katika takriban miaka 70, huku kikiwa ni kipigo kizito zaidi walichopigwa kikosi cha Simba watatu wakiwa katika uwanja wa nyumbani tangu walipofungwa 6-1 na Scotland mwaka 1928.

Matokeo hayo yanaleta mazingira magumu ya michezo ya mwisho ya UEFA Nations league, ikumbukwe England ilipoteza mchezo wa kwanza mjini Budapest kwa bao 1-0 mwezi huu, kabla ya kutoka sare na Ujerumani na Italia, kisha jana kupoteza tena wakiwa nyumbani.

England wanaburuza mkia katika Ligi A kundi la 3 la Michuano hiyo ya Mataifa ya Ulaya wakiwa na alama mbili tu, huku Hungary wakiongoza kundi hilo wakiwa na alama 7 na kufatiwa na Ujerumani wenye alama 6, huku Italia wakishika nafasi ya 3 wakiwa na alama 4.