Jumatatu , 31st Mar , 2014

Kamati ya Sheria na hadhi za Wachezaji ya shirikisho la la soka nchini Tanzania TFF, imekutana Ma

Kamati ya Sheria na hadhi za Wachezaji ya shirikisho la la soka nchini Tanzania TFF, imekutana Machi 30 mwaka huu kujadili utekelezaji wa maagizo ya TFF kwa wanachama wake, ikiwa ni pamoja kurekebisha Katiba zao ili ziendane na Katiba ya TFF pamoja na ile ya FIFA kabla ya Machi 30 mwaka huu.

Kamati hiyo imekatakaa pendekezo la wanachama wa Simba kubadili kipengele na 26 kuhusu sifa za mgombea ambacho kilikuwa kinazuia mgombea ambaye ametumikia kifungo kutogombea kinapingana na kipengele na 29 (4) cha Katiba ya TFF

Mchakato wa uchaguzi wa Klabu ya Simba uendelee kama ulivyopangwa, wakizingatia uamuzi wa Kamati hiyo ambapo TFF inaitakia Klabu ya Simba kufanya uchaguzi mwema.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, pia imeshauri TFF kuwasiliana na FIFA kupata mwongozo kuhusu katazo la watu wenye rekodi ya kifungo, kugombea katika uchaguzi.