Viongozi wa vyama vya mpira wa miguu kwa wanawake mikoani wametakiwa kuandaa mashindano mbalimbali ya wanawake ili kuweza kukuza soka kwa upande wa wanawake hapa nchini.
Akizungumza na East Africa Radio, Kocha wa Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars, Rogasian Kaijage amesema viongozi hao wanatakiwa kutumia michezo hiyo ikiwemo ya Taifa Cup inayotarajiwa kuanza mwakani ili kuweza kuibua vipaji vipya vya vijana mbalimbali nchini.
Kaijage amesema hivi sasa timu ya wanawake imekosa hamasa kutokana na viongozi hao kushindwa kusimamia mashindano mbalimbali kwa ajili ya kuweza kukuza na kupata vipaji vipya.
Kaijage amesema uundwaji wa timu za wanawake inategemea na mashindano mbalimbali yakiwemo ya vijana ili kuweza kukua na vijana hao ambao watakuwa na uwezo wa kutumikia timu kubwa za ndani na nje ya nchi.