Jumatatu , 18th Jun , 2018

Nyota wa Yanga Juma Mahadhi ameweka wazi mipango yake kuwa huenda akabaki au akaondoka Yanga, lakini  mipango yake na wakala wake inayoendelea sasa ndo  itaamua hatima yake ya msimo ujao.

Mahadhi ameeleza hilo Jumamosi iliyopita kwenye kipindi cha Shabiki On Saturday cha East Africa Television, ambapo pia aliweka wazi mipango yake ya kucheza soka nje ya Tanzania.

''Bado nina mkataba na Yanga nitaendelea kuwepo lakini nina mipango ya kucheza soka nje ya nchi na mipango inaendelea hivyo chochote kinaweza kutokea ila kwasasa bado nipo Yanga'',. amesema Mahadhi.

Mahadhi mwenye umri wa miaka 21 amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu aliposajiliwa na Yanga akitokea klabu ya Coastal Union. Licha ya kutopata nafasi ya kutosha chini ya kocha Lwandamina, lakini amekuwa akionesha uwezo kila anapopata nafasi.

Mahadhi pia amesema hawezi kuondoka Yanga kwasababu ya ukame wa pesa uliopo sasa, bali kazi yake ni kucheza uwanjani na kuhakikisha timu inafanya vizuri ili klabu ipate wadhamini na pesa ziingie kwa wingi.