
Julio amesema, mara nyingi anaziogopa timu zote isipokuwa Simba, Yanga na Azam kwasababu anaamini timu zote zilizopo ligi kuu ambazo sio kubwa zina uwezo wa kufanya vizuri ili kuweza kufikia nafasi ambazo wanazitarajia.
Kwa upande wake mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Simon Msuva ambapo hapo kesho wanashuka dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kukipiga dhidi ya Mbeya City amesema, wamefanya maandalizi mazuri na wanaamini kila mechi kwao ni fainali na ushindi katika mechi ya kesho utawasaidia kuweza kufanya vizuri zaidi katika mechi zinazofuata.