Jumamosi , 15th Mei , 2021

Michuano ya Basketbal Afrika League (BAL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Jumapili ikishirikisha timu 12 kutoka barani Afrika.

Rapa J.Cole(Pichani) anatarajiwa kuonesha umwamba wake kwenye michuano ya BAL itakayoanza kutimua vumbi kesho nchini Rwanda.

Mechi ya ufunguzi itakayopigwa kesho ni  ile itakayoihusisha timu mwenyeji Patriots ya Rwanda itacheza dhidi ya Hoopers ya Nigeria huku Kivutio kikubwa zaidi katika michuano hii ni nyota wa muziki wa Rap, J.Cole ambaye amesaini na timu ya Rwanda Patricots B.B.C na kesho anatazamiwa kuwa dimbani.

J.Cole aliwasili nchini Rwanda Mei 8 mwaka huu ili kujiweka karantini ili ashiriki katika michuano hiyo ambapo anatarajiwa kucheza michezo mitatu hadi sita akiwa na Patriots ya Rwanda.

Mashindano hayo yana timu 12 ambapo Sita zinawakilisha mabingwa wa nchi za Angola, Misri, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia, wakati zingine sita zilifika fainali kupitia raundi za kufuzu. Walakini,kwa sababu ya janga la Covid-19 mfumo wa mashindano umebadilishwa na sasa ina makundi matatu ambapo kila timu itacheza na timu nne.

Timu mbili za juu zitasonga mbele kwa mchujo, wakati maeneo mengine mawili yatatengwa kwa vilabu viwili vya juu vilivyoshika nafasi ya tatu.(Mshindwa bora)

Vilabu shiriki katika michuano hiyo ni wenyeji Patriots(Rwanda) Zamaleki(Misri), US Monastir (Tunisia), AS Salé (Morocco), AS Douanes (Senegal), Rivers Hoopers (Nigeria), Petro de Luanda (Angola), GNBC (Madagascar), Ferroviário (Mozambique), Patriots (Rwanda), GSP (Algeria), AS Police (Mali) and FAP (Cameroon).

Hapo awali, timu kumi na mbili zilitakiwa kugawanywa katika mikutano miwili ambayo inacheza michezo mitano kila moja. Timu tatu za juu kutoka kila mkutano zingekuwa zimesonga mbele kwa Super 6.

Mechi nyingine ni kati ya AS Douanes ambao mei 17 watamenyana dhidi ya GSP ya Algeria, Zamaleki ya Misri nayo itapepetana na Ferroviario Maputo ya Msumbiji wakati siku hiyo hiyo US Monastir ya Tunisia itakipiga dhidi ya GNBC kutoka Madagascar.

Mei 18 itashuhudiwa Petro de Luanda ya Angola itaoneshana ubabe dhidi ya AS Police ya Mali, nayo AS Sale ya Morocco watakipiga dhidi ya FAP ya Cameroon.

Michuano hiyo itafikia tamati Mei 19, ambapo GNBC itakabiliana na Patriots,Maputo watamenyanja na AS Douanes nayo Zamaleki itacheza dhidi ya GSP.