Alhamisi , 8th Mei , 2014

Michuano ya mpira wa kikapu kwa majiji ya Afrika Mashariki na Kati ijulikanayo kama Intercity inazidi kushika kasi kwa timu mbalimbali kuchuana.

Michuano ya mpira wa kikapu kwa majiji ya nchi za Afrika Mashariki na kati Intercity inayofanyika jijiin Dar es salaam imeendelea hii leo kwa michezo mbalimbali kupigwa kwa timu tofauti kuchuana vikali katika mechi zinazochezwa katika uwanja wa ndani wa taifa.

Katibu mkuu wa Intercity Ronnie Owino amesema pamoja na uchache wa timu lakini ushindani katika michuano hiyo msimu huu ni mkubwa mno na pia waamuzi wamekua wakichezesha kwa kufuata kanuni na hivyo kupunguza malalamiko kutokana na maamuzi yao.

Naye mmoja wa wachezaji mahiri wa timu ya wanawake wa jiji la Dar es salaam Tukusubira David anasema timu za wanawake zimejiandaa vizuri kitu kinachopelekea michezo yao kuwa migumu mno.