Jumanne , 1st Sep , 2020

Tarehe na mwezi kama huu mwaka 2013,Klabu ya Real Madrid ilimtambulisha Gareth Bale baada ya kumsajili akitokea Tottenham Hotspurs ya Uingereza kwa dau la paundi milioni 91.

Safu kali ya ushambuliaji ya Real Madrid iliyokua imeundwa na Cristiano Ronaldo (Wa kwanza kushoto), Gareth Bale (Kati) na Karim Bemzema(Kulia) wakishangilia bao katika moja ya mchezo.

Usajili huo ulimfanya Bale kuwa mchezaji ghali zaidi duniani akiipiku rekodi ya uhamisho wa Cristiano Ronaldo aliyejiunga na wababe hao wa Ulaya kwa dau la pauni mlioni 80 mwaka 2009 akitokea Manchester United ya Uingereza.

MAFANIKIO YA BALE NDANI YA REAL MADRID

2014-Taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya

2014-Taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya

2017-Taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya

2018-Taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya

2016/17-Taji la Ligi Kuu ya Hispania

2019/20-Taji la Ligi kuu ya Hispania

 

USICHOKIJUA KUTOKA KWAKE.

Gareth Bale ambaye ni raia wa Wales alikua akicheza kama beki wa kushoto katika Klabu ya Southampton na aliibuka kuwa mpigaji mzuri wa mipira ya adhabu .

Alijiunga na Southampton mwaka 1999 tangu akiwa mdogo hadi mwaka 2006 na mwaka uliofuata ndipo alijiunga na Spurs.

Mwaka 2007 alijiunga na Totetenham Hotspurs iliyokua ikinolewa na kocha Harry Redknapp kwa ada ya uhamisho kiasi cha paundi milioni 7 tu.

NAMBA ZAKE ZINAVUTIA

Licha ya kuwa na mgogoro kwa hivi sasa na kocha wake Zinedine Zidane,Bale alikua na wastani mzuri wa kupachika mabao.

Mechi -251

Mabao-105

UTATU MTAKATIFU

Ujio wa Gareth Bale ndani ya Real Madrid, ulitengeneza safu bora ya ushambuliaji iliyowajumuisha yeye Bale, Karim Bemzema na Cristiano Ronaldo iliyofahamika kwa jina la BBC ambayo ilishindana vilivyo na ile ya akina Lionel Messi,Luis Suarez na Neymar Jr ya Barcelona maarufu kama MSN ambao kila kukicha walikua wakipachika mabao.

TAKWIMU ZAKE NDANI YA BBC

2014/15

-Mechi 148

-Bao 100

-Assists 46

Bale alicheza mechi 31,Bao 13 na Assists 9

2015/16

-Mechi 115

-Bao 98

-Assists 34

Bale alicheza mechi 23,Mabao 18 na Assists 10

2016/17

-Mechi 120

-Bao 70

-Assits 22

Bale alicheza mechi 19,Mabao 7na Assists 2

Je Zidane anaipoteza thamani yake?