
Kaimu katibu mkuu wa RT Ombeni Zavara amesema, wamepokea barua kutoka shirikisho la riadha duniani IAAF wakiwataka kuandaa kambi ya vijana watakaokuwa katika mafunzo maalumu ambapo IAAF imesema itagharamia kila kitu katika mafunzo hayo kwa kila mwaka kuanzia mwakani.
Zavara amesema wanajitahidi kutafuta watoto ambao watakuwa na vipaji vya mchezo wa riadha ambao watapata mafunzo ndani ya kambi wakiwa na walimu maalumu ambao watawawezesha kuwa wanariadha wazuri na watakaoweza kuipeperusha bendera ya nchi katika mashindano mbalimbali.
Zavara amesema, mpaka sasa zipo shule mbili zinazotoa mafunzo ya michezo ambayo ni Filbert Bayi na Lord Badden ambapo kwa upande wa shule nyingine zinaishia kushiriki mashindano ya UMITASHUMTA na baada ya hapo hawaendelei na masomo yoyote hivyo kwa kuwa na kambi itasaidia kuwawezesha vijana kujiendeleza katika michezo.