
moja ya matukio kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza Simba Vs Kaizer Chiefs
Kufuatia ushindi wa bao 4 - 0 siku saba zilizopita katika dimba la FNB Afrika Kusini, Kaizer Chiefs wanaingia kwenye mchezo wa jioni ya leo katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es salaam wakiwa na nafasi kubwa zaidi ya kusonga mbele na kuendelea kuandika historia kwenye michuano hii ambpo pia hii ni mara yao ya kwanza kufika hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika.
Wekundu wa Msimbazi Simba wanahitaji ushindi wa mabao 5-0 ilikujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza.
Miaka 47 iliyopita mwaka 1997 klabu ya Simba ili pindua matokeo na kusonga mbele kwenye michuano hii ya vilabu barani Afrika dhidi ya Mufurila Wonders ya Zambia ambapo mchezo wa kwanza Simba ilifungwa bao 4-0 lakini mchezo wa pili walipindua matokeo na kushinda 5-0 na kusonga mbele.
Ni Jonas Mkude pekee ndio mchezaji atakao kosekana katika mchezo wa leo kwa upande wa Simba kutokana na matatizo binafsi, lakini wachezaji wote wapo vizuri hakuna mwenye majeruhi wala mwenye adhabu itakayo mfanya akose mchezo huu.
Kwa upande wa Kaizer Chiefs golikipa wao Itumeleng Khune anarejea kwenye kikosi baada ya kupona maumivu ya bega, lakini Dumisani Zuma ambaye aliumia kwenye mchezo wa kwanza ataendelea kukosekana pamoja na mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Khama Billiat.
Mchezo huu unachezwa leo Saa 10:00 jioni katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es salaam.