Jumamosi , 13th Mei , 2017

Mbeya City imesema haitaki kuwa ngazi ya Yanga kutwaa ubingwa hivyo watahakikisha hawapotezi mechi ya leo itakayopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mechi ya raundi ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, timu hiyo iliibuka kidedea dhidi ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu, Yanga. 

Kocha wa Mbeya City Kinna Phiri alisema mchezo wao dhidi ya Yanga utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wao hao kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao, lakini hawatakubali kuwa ngazi. “Tumefanya maandalizi mazuri na tumerudi kutoka Sumbawanga, ambako tuliweka kambi ya siku tano na kucheza michezo minne ya kirafiki, ambayo tulishinda yote,” alisema Phiri.