Jumanne , 8th Oct , 2024

Kocha wa Manchester United hatima yake katika kikosi cha Mashetani Wekundu kujulikana leo baada ya kikao cha zaidi ya masaa mawili walichokaa Mabosi wa United siku ya jana Oktoba 7/ 2024 kujadili muenendo wa timu hiyo ambayo haijapata matokeo ya ushindi katika michezo mitano mfululizo

Ten Hag amejiunga United 2022 na kuiongoza timu hiyo kutwa kombe la ligi 2023, FA 2024 kocha huyo raia wa Uholanzi alisaini mkataba wa kubaki kwa Mashetani Wekundu kwa mwaka mmoja zaidi mwezi Juni 2024

Hatima ya Eric Ten Hag kwenye  kikosi cha Manchester United itajulikana leo siku ya Jumanne baada ya kikao cha muda mrefu walichokaa Mabosi wa Mashetani Wekundu kujadili muenendo wa kikosi chao.

Jana Oktoba 7/2024 Mabosi wa United waliketi kwa zaidi ya masaa mawili makao makuu ya klabu kujadili kuhusiana na matokeo ya timu  na namna inavyocheza kwa ujmla. Jumapili Oktoba 6, 2024 Villa Park  kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza Mabosi wote wa kikosi hiko  walionekana jukwaani kuitizama timu yao.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema inawezekana muda wowote siku ya Jumanne Oktoba 8/ 2024 Viongozi wakatoa tamko rasmi juu ya hatima ya kocha wao raia wa Uholanzi Eric Ten Hag aliyeongeza mkataba wa kusalia kwenye viunga vya Old Trafford kwa mwaka mmoja zaidi  mwezi Juni.

Ten Hag aliyewahi kufundisha timu ya Ajax Amstedam ameiwezesha United kutwaa ubingwa wa kombe la ligi 2023 na kombe la FA 2024. Mabosi wa United hawaridhishwi na jinsi timu  inavyocheza hali hii imetokana na kocha kupewa wachezaji aliokuwa akiwahitaji kujenga kikosi chake lakini bado mambo hayabadiliki.

Mara ya mwisho United kushinda ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza ilikuwa msimu wa 2012-2013 chini Sir Alex Ferguson, katika michezo mitano ya hivi  karibuni mabingwa wa kombe la mabingwa barani Ulaya 2007-2008 hawajapata matokeo ya ushindi hivyo kupeleka presha kubwa kwa mkufunzi wa Mashetani Wekundu.

Ruud Van Nistelroy anatizamwa kama mtu sahihi kukaimu nafasi ya kocha mkuu wa Mabingwa hao  wa kistoria ligi kuu nchini Uingereza wenye makombe 20. Thomas Tuchel, Massimiliano Allegri,Simone Inzaghi wanahusishwa kujiunga na timu hiyo endapo Ten Hag atafutwa kazi.