Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Hasira zetu zimetuponza- Kocha Evans

Jumatatu , 21st Aug , 2017

Kocha wa timu ya TMT, Evans Davies Mwaseba amefunguka na kudai sababu iliyopelekea mpaka timu yake kufungwa katika 'game 3' kwa pointi 87-82 ni kutokana na wachezaji wake kuhamaki baada ya kuchezewa faulu sana na wapinzani wao.

Kocha wa timu ya TMT, Evans Davies Mwaseba.

Mwaseba ameeleza hayo baada ya timu yake kuonekana kuzidiwa katika robo ya nne ya mchezo wa fainali uliyochezwa katika viunga vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam na kusababisha kuwaruhusu wapinzani wao waendelea kupachika mpira katika goli lao.

"Kilichosababisha tufungwe katika 'game 3' na Mchenga BBall Stars ni kutokana sisi kuhamaki kuanzia kwenye benchi la wachezaji mpaka wale waliyokuwa ndani wakicheza baada ya kuona wakichezewa faulo nyingi, lakini tunaenda kujipanga vizuri kuelekea mechi ijayo ya game 4 ili tuweze kufanya mashabulizi vizuri na tuweze kuziba mapungufu yaliyoweza kujitokeza katika mechi iliyopita", alisema Mwaseba.

Pamoja na hayo, TMT mpaka sasa imeweza kushinda mechi 1 na kufungwa 2 katika fainali hizi zinazoendelea huku mpinzani wake Mchenga BBall Stars akiwa ameshinda mechi 2 na kupoteza mechi 1.

Mshindi wa kwanza katika fainali za Sprite BBall Kings anatarajiwa kuondoka na kitita cha Milioni 10 huku mshindi wa pili kuondoka na Milioni 3 na kumaliziwa na mchezaji bora 'MVP' kupata Milioni 2.

HABARI ZAIDI

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao