
Mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga, Haruna Moshi 'Boban'.
Akizungumza na EATV Boban amesema yoyote atayekuwa amejianda vizuri atashinda ila ni ngumu kutabiri yupi atashiinda kutokana na ugumu wa mechi hizo.
''Mandalizi ya Simba na Yanga yanakuwa ya kipekeake kutokana na mara nyingi viongozi wanakuja kambini kukaa na sisi kutupa maneno namna gani ambayo tutacheza na pia kutupa ahadi iwapo tutashinda".
Hata hivyo Nyota huyo wa zamani wa timu ya Taifa 'Taifa stars' Boban ijumaa ya wiki hii atahitimu mafunzo ya kozi ya FIFA ya Grassroots ambayo yanasimamiwa na mkufunzi kutoka katika shirikisho la mpira wa miguu nchini Raymond Gweba .