Jumamosi , 15th Mei , 2021

Kocha Thomas Tuchel amewaambia wachezaji wake wa Chelsea hakutakuwa na wakati wa kusherehekea ikiwa wataifunga Leicester City katika fainali ya Kombe la FA leo, kwa sababu lazima waanze mara moja maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya wapinzani hao hao utakao chezwa Jumanne Mei 18, 2021

Thomas Tuchel

The blues wana nafasi ya kutwaa ubingwa wa kwanza chini ya kocha huyo raia wa Ujerumani ambaye alijiunga na kikosi hicho mwezi Januari mwaka huu akichukua nafasi ya Frank Lampard, lakini bado kikosi hicho hakijajihakikishia nafasi ya kumaliza kwenye nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu nafasi ambayo itawapa tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya msimu ujao.

kuelekea Michezo miwili inayofuata dhidi ya Leicester City mmoja ukiwa ni wa fainali ya kombe la FA leo usiku na mwingine wa Ligi Kuu siku ya Jumanne Mei 18 2021, kocha Thomas Tuchel amesema,

"Hakuna sherehe, hakuna sherehe zilizopangwa. Hizi ni nyakati maalum ikiwa tutashinda hakuna kilichopangwa, ni karibu sana tutacheza tena Jumanne. Hali katika ligi hairuhusu sisi kusherehekea, tuna fainali mbili zinazokuja na tunataka kushinda zote mbili. leo itakuwa na athari kubwa mwilini na tunahitaji kuwa tayari Jumapili kufanya kikao kizuri cha kupona na Jumatatu kujiandaa na michezo ijayo, ikiwa kuna sherehe, tunahitaji kuwachelewesha kidogo."

Kipigo cha bao 1-0 walichokipata Cheslea dhidi ya Arsenal na ushhindi wa bao 4-2 walioupata Liverpool dhidi ya Manchester United unaifanya Chelsea kuwa na tofauti ya alama 4 tu dhidi ya majogoo hao wa Anfield walio nafasi ya tano wakiwa na alama 60, wakati Chelsea wenye alama 64 wamecheza mchezo mmoja zaidi ya Liverpool, hivyo ikitokea majogoo hao wa Anfield wakishinda mchezo huo tofauti yao na chelsea itakuwa ni alama moja tu.