Haji Manara
Kifaru amesema hayo leo kupitia kipindi cha Kipenga Xtra, cha East Africa Radio kinachoruka kila siku za Jumatatu mpaka Ijumaa, kuanzia saa 6:00 hadi saa 7:00 mchana, ambapo ameweka wazi kuwa aliahidiwa simu kwaajili ya kuitumikia kwenye mambo ya mitandao.
''Manara namdai simu yangu aliniahidi akitoka Uturuki ataniletea ili na mimi niingie mitandaoni japo nilikuwa sitaki haya mambo ya mitandao. Kupitia Kipenga Xtra naomba anisikie kuwa leo nataka tukutane anipatie simu yangu'', Kifaru.
Kifaru alisema ahadi hiyo ya simu imetokana na uhusiano wake mzuri na wasemaji wanaochipukia baada ya yeye kufanya vizuri kwa muda mrefu zaidi kwenye kazi hiyo hivyo amejijengea uhusiano mzuri na wasemaji wengine.
Thobias Kifaru akiwa studio za East Africa Radio kwenye kipindi cha Kipenga Xtra
Pamoja na kutupiana maneno mengi wakati vilabu vyao vinapokutana kwenye mechi mbalimbali, Kifaru amesema wasemaji ni marafiki na huwa wanakutana mara kwa mara tofauti na watu wanavyoweza kudhani.