Jumapili , 18th Jan , 2015

Kocha wa Simba, Mserbia Goran Kopunovic amesema kwa hawezi kugawanya wachezaji katika timu hiyo hata kama kuna wachezaji wa kimataifa na wazawa.

Akizungumza na East Africa Radio, Goran amesema kwa anaona wachezaji wote wanauwezo sawa kutokana na nafasi wanazocheza na kila mchezaji anajituma kwa manufaa ya timu hivyo hajaona utofauti kati ya wachezaji hao.

Gorana mesema,kila mchezaji anamkataba wake wa kazi na anajua ni nini anatakiwa kufanya anapokuwa uwanjani hivyo haoni haja ya kugawanya makundi ya wachezaji wa kimataifa na wachezaji wazawa.

Goran amesema, Simba ni timu kubwa na atahakikisha inakuwa kubwa zaidi kwa kuweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimba ya ndani na nje ya nchi.