Ijumaa , 27th Mei , 2022

Timu ya Golden State Worriors imefuzu fainali ya Ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA kwa mara ya kwanza tangu 2019

Golden State Worriors imeshinda mchezo wa 5 (game 5) ya fainali kanda ya Magharibi  leo alfajiri dhidi ya Dallas Maverick kwa ushindi wa alama 120 kwa 110 na kuongoza 4-1 kwenye michezo 5 kati ya michezo 7 ya fainali.

Kwa ushindi huu Golden state ndio mabingwa ukanda wa Magharibi na wamefuzu kucheza fainali ya NBA msimu huu. Na watacheza na mshindi wa ukanda wa Mashariki kati ya Boston Celtcs au Miami heat.

Katika mchezo huu Klay Thompson wa Golden State Worriors amefunga points 32 Rebound 2 na pasi za kufunga (Assists) 3. Stephen Curry amefunga alama 15 pasi za kufunga (Assist) 9 na Rebound 3.