
Tyson Fury (Kulia) akimuadhibu Diontay Wilder (Kushoto) katika moja ya pigano walilokutana uliongoni.
Fury mwenye umri wa miaka 32, ameonekana akimamilisha pambano la kuwania mataji yote manne ya ulimwengu dhidi ya Antony Joshua huko Saudi Arabia.
Mwanamasumbwi huyo alihudhuria kwenye ushindi wa Josh Taylor dhidi ya Jose Ramirez huko Las Vegas Jumamosi ambapo ndipo alisaini mkataba wake wa pigano dhidi ya Wilder.
Kabla ya hapo ilidhaniwa kuwa Fury angepigana na Antony Joshua ambaye anatarajiwa kutetea mikanda yake ya IBF, WBA na WBO dhidi ya Oleksandr Usyk wa Ukraine mnamo Agosti mwaka huu,
Fury alimpiga Wilder kumaliza utawala wake kama bingwa wa WBC huko Las Vegas mnamo Februari 2020,ikiwa ni miezi 14 baada ya wababe hao kutoka sare kwenye pigano lililofanyika Los Angeles.
Ukumbi kwa ajili ya pigano hilo lao la tatu bado haujatajwa ingawa upande wa Fury ulipendekeza lifanyikie Las Vegas ambao unachukua takribani mashabiki 65000.