Ijumaa , 24th Jun , 2022

Shirikisho la soka Duniani FIFA limethibitisha kuwa litaruhusu timu zinazoshiriki michunoa ya kombe la dunia kuongeza wachezaji hadi kufikia wachezaji 26 katika vikosi vyao kwa ajili ya michuano hiyo itakayofanyika nchini Qatar mwezi November mwaka huu.

Gianni Infantion - Rais wa shirikisho la soka Duniani (FIFA)

Hapo awali timu ziliruhusiwa kuwa na wachezaji 23 pekee kikosini, lakini shirikisho hilo limeongeza idadi ya wachezaji watatu kutokana na kuendelea kuwepo kwa janga la COVID-19 hivyo ongezeko hilo litawezesha timu kupata machaguo zaidi endepo baadhi ya wachezaji watakutwa na maambuki ya virusi vya corona kulazimika kujitenga kwa muda.

Tarehe ya mwisho kwa nchi zote 32 zitakazoshiriki michuano hiyo kuwasilisha majina ya vikosi vyao ni tarehe 20 Oktoba 2022 ambayo ni siku 30 kabla ya mchezo wa kwanza wa michuano hiyo kati ya Senegal na Uholanzi mchezo utakaopigwa kwanye uwanja wa Al Thumama uliopo kilomita 12 kusini mwa jiji la Doha nchini Qatar.

Vile vile Shirikisho hilo la soka Duniani FIFA kwenye taarifa hiyo wameongeza kusema kuwa wachezaji 15 wataruhusiwa kuwekwa kwenye orodha ya wachezaji wa akiba katika mchezo huku benchi la ufundi likiwa na jumla ya watu 11 lakini mmoja wao lazima awe ni daktari.