
Felix amesema hivi karibuni alikuwa amesimama kwa muda kufanya mazoezi kutokana na kuumia mguu lakini wiki iliyopita alipata nafuu na anaendelea na mazoezi yake jijini Arusha akiwa pamoja na wanariadha wengine akiwemo Fabian Joseph aliyekuwa kituo cha kimataifa cha Kep Keino nchini Kenya ambaye kwa sasa yupo nchini kwa ajili ya mapumziko.
Felix amesema, hatarajii kufanya mazoezi chini ya kocha yeyote kwa kuwa hana uwezo wa kulipa kutokana na kuwa mchezaji binafsi, hivyo atasubiri kambi ya taifa mara tu shirikisho la Riadha Tanzania RT litakapoamua kufanya hivyo.