Feisal Salum
Kiungo huyo ametwaa tuzo hiyo akiwashinda Moses Phiri mshambuliaji wa Simba na Relliats Lusajo wa Namungo.
Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imeeleza kuwa mchezaji huyo alichaguliwa kutokana na kuonyesha uwezo mzuri ndani ya Septemba.
Kwa upande wa kocha ni Honour Janza wa Namungo yeye amewashinda Hitimana Thiery wa Namungo na Charles Mkwasa wa Ruvu Shooting.
Fei alitupia mabao mawili ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Mkapa na ubao ulisoma Yanga 2-2 Azam FC.