Jumapili , 29th Jan , 2017

Roger Federer ametwaa taji lake la18 la Grand Slam, na la kwanza baada ya miaka 5 kupita, kwa kumchapa Rafael Nadal kwa jumla ya seti tano kwenye fainali ya mashindano ya wazi ya Australia hii leo.

Roger Federer baada ya kukabidhiwa taji lake

 

Federer mwenye umri wa miaka 35, raia wa Uswisi, alishinda kwa 6-4 3-6 6-1 3-6 6-3 na kutwaa taji hilo kwa mara ya tano na kuingia katika orodha ya mabingwa wa muda wote kwa upande wa wanaume.

Federer alikuwa kwenye ukame wa mataji kwa miaka mitano, na taji lake la mwisho ni la mashindano ya Wimbledon mwaka 2012.

 

Hadi sasa tangu mwaka 2006 Federer na Nadal wamekutana katika fainali 9 ambapo Nadal ameshinda katika fainali 6