Jumatano , 25th Nov , 2015

Timu ya mpira wa wavu ya ufukweni ya Jeshi Stars na IP Sports kwa upande wa wanaume na Tanzania Prisons na Makongo B kwa upande wa wanawake zinatarajia kukutana leo katika mchezo wa fainali utakaopigwa katika uwanja wa JK Park jijini Dar es salaam.

Mjumbe wa kamati ya Chama cha Wavu Mkoa wa Dar es salaam DAREVA Nassor Sharrif amesema, wanatarajia kuunda kikosi cha wachezaji 11 kutoka katika ligi hiyo iliyoanza kutimua vumbi Septemba mwaka huu.

Sharrif amesema, wamempa kazi kocha wa timu ya mkoa kuangalia wachezaji anaowahitaji na wanaamini baada ya kumalizika kwa mashindano hayo watapokea orodha ya majina ya wachezaji wengine watakaokluwa wamechaguliwa.

Jeshi Stars ilifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kuifunga Tanzania Prisons Seti 2-0 wakati IP Sports ikiwachapa Chui kwa Seti 2-0 pia.

Kwa upande wa wanawake, timu ya Tanzania Prisons ilitinga fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Shule ya Sekondari ya Makongo kwa Seti 2-0 huku Shule ya Makongo A ikiwafunga ndugu zao Makongo B kwa Seti 2-0.