Alhamisi , 3rd Dec , 2015

Kocha Mkuu wa Timu ya Tanzania Bara The Kilimanjaro Stars, Abdallah Kibadeni amesema Ethiopia haikuwa na uwezo wa kukifunga kikosi chake, lakini walibebwa na CECAFA

Kibadeni amesema CECAFA ilionyesha wazi ilitaka kuona Ethiopia wanafika mbali licha ya kuwa na kikosi kibovu.

Kibadeni amesema hakuwampanga Mlinda Mlango Aishi Manula pamoja na mshambuliaji Elius Maguli katika mechi ya pili ya Ethiopia hatua ya robo fainali kwa kuwa walikuwa na kadi mbili za njano huku Ally Mustapha Barthez naye akiwa mgonjwa.

Stars imewasili hapo jana ambapo ilimaliza mechi zote mbili dhidi ya Ethiopia kwa sare ya 1-1 lakini hatua ya robo fainali ikatolewa kwa mikwaju ya penalti 4-3.