
Wachezaji wa Timu ya taifa ya wanawake ya England
Uhispania wana kikosi kilichojaa washindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, na ni moja kati ya timu zinazopigiwa upatu kutwaa Ubingwa hata kabla ya michuano hiyo kuanza. England wao wana faida ya kucheza nyumbani katika mji wa Brighton, katika mchezo huo wa kuwania nafasi ya kufuzu nusu fainali.
Imani imeongezeka kwa kikosi cha wenyeji England, waliyo orodheshwa katika nafasi ya nane kwenye viwango vya ubora duniani, wakiwa nyuma kwa nafasi moja tu na Uhisapania, wakiwa wamecheza michezo 17 mfululizo bila kufungwa tangu Mholanzi Sarina Wiegman achukue nafasi ya Kocha Mkuu kukinoa kikosi hicho mwezi Septemba mwaka 2021.
England ilishinda michezo yote mitatu katika hatua ya makundi bila kuruhusu bao hata moja, huku wakifunga magoli 14 na kuipiku rekodi ya awali ya michuano hiyo ya ya kufunga magoli 11 iliyowekwa na Ujerumani mwaka 2011.
Ushindi wa mabao 8 kwa 0 walioupata dhidi ya Norway katika mchezo wao wa pili, nao ndio ulikuwa ni ushindi mkubwa zaidi katika historia ya michuano hiyo.