Jumatatu , 14th Nov , 2016

Klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund imesema kuwa mwanariadha wa mbio fupi kutoka Jamaica Usain Bolt atashiriki katika mazoezi na klabu hiyo kwa siku chache.

Usain Bolt

 

Bolt mshindi wa medali 9 za dhahabu kwenye mashindano ya matatu ya Olimpiki, amesema anataka kustaafu mwakani baada ya mashindano ya London, ya kipindi cha kiangazi, na baada ya hapo atacheza soka.

Wakimkaribisha nyota huyo, maafisa wa klabu hiyo wamesema kuwa hakuna hakikisho kwamba mwanariadha huyo ataichezea klabu hiyo katika siku za usoni.