Jumanne , 7th Jun , 2016

Usajili wa wachezaji kwa vilabu vya Ligi kuu nchini Tanzania unatarajiwa kifunguliwa Juni 15 ikiwa ni kipindi cha uhamisho wa wachezaji utakaokamilika Agosti sita.

Afisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF Alfredy Lucas amesema, pingamizi litaanza Agosti saba mpaka 14 ambapo vilabu vitatakiwa kuthibitisha usajili wa kwanza kati ya Agosti 15 na 19 huku usajili wa awamu ya pili ukianza Agosti 17 mpaka Septemba saba.

Lucas amesema, kipindi cha pingamizi kwa hatua ya pili kitaanza Septemba nane mpaka 14 huku Septemba 15 mpaka 17 ikiwa ni siku za kuthibitisha usajili kwa vilabu.

Lucas amesema, timu zinatakiwa kuandaliwa kuanzia June 15 mpaka Julai 15 ambapo kuanzia Julai 16 mpaka Agosti nne ni kipindi cha timu kuwa na miechi za kirafiki za ndani na nje ya nchi huku ratiba ya Ligi kuu ikitarajiwa kutoka kuanzia kati ya Julai 16 mpaka Agosti 14.

Kwa upande mwingine Lucas amesema, Kamati ya utendaji ya TFF imeteua kamati ya lesenia mbayo ndiyo yenye jukumu la kupitia maombi ya leseni kwa klabu za Ligi kuu na Ligi daraja la kwanza.

Lucas amesema, Klabu zinatakiwa kuchukua fomu za maombi za TFF ambapo baada ya kuzirejesha zitafanyiwa kazi na zile zitakazokuwa zimekidhi matakwa ya kanuni husika zitapatiwa leseni husika.

Lucas amesema, lengo la kuwa na leseni kwa vilabu ni kuhakikisha mpira wa miguu unaendeshwa kwa weledi na kupiga vita upangajai wa matokeo katika maeneo matano ambayo ni wachezajio, viwanja, utawala, umiliki wa klabu na fedha.

Lucas amesema, vilabu vinatakiwa kutuma maombi mapema ili kutoa nafasi kwa TFF kuyafanyia kazi huku klabu ambayo haitapata leseni kwa kutokidhi vigezo ikiruhusiwa kukata rufaa.

Wajumbe walioteuliwa kusimamia kamati hiyo ni Wakili Loid Nchunga ambaye atakuwa ni Mwewnyekiti, Wakili Emmanuel Matondo akiwa makamu mwenyekiti, David Kivembele, Hamisi Kisiwa na Profesa Mshindo Msola wakiwa ni wajumbe wa kamati hiyo.