Jumanne , 15th Dec , 2015

Vilabu Shiriki vya Ligi nchini vimetakiwa kuzingatia sheria na kanuni za kuendesha Ligi katika zoezi zima la ufungaji wa Dirisha Dogo la usajili linalotarajiwa kufungwa leo saa sita usiku.

Afisa habari w aShirikisho la Soka nchini TFF Baraka Kizuguto amesema, kutakuwa na wiki moja kwa ajili ya pingamizi na baada ya hapoi kamati ya sheria na hadhi za wachezaji itapitia usajili ambapo baada ya hapo wachezaji hao wataweza kutumika kwa timu husika zilizotumia utaratibu unaotakiwa katika usajili.

Kizuguto amesema, kamati ya sheria na hadi za wachezaji inatarajia kukutana Desemba 23 mwaka huu kwa ajili ya kupitia usajili wote wa dirisha dogo na kutakachopitishwa kitatolewa taarifa kwa ajili ya kuanza rasmi kutumika kwa wachezaji hao.