Jumatano , 8th Jul , 2020

Mdau na mwanachama wa klabu ya Simba ,Azim Dewji ameshauri mchezo wa nusu fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup kati ya Simba na Yanga kupelekwa mbele kwa wiki moja mbele ili kupisha tukio la mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi CCM .

Aliyekua mfadhili wa klabu ya soka ya Simba,Azim Dewji(pichani)

Aliyewahi kuwa mfadhili wa klabu ya Simba,Azim Dewji ameliomba shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kuupeleka mbele mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga kwa wiki moja zaidi ili kupisha mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi CCM ambao utafanyika siku hiyo ya mchezo.

Dewji ameyasema hayo wakati matayarisho ya mchezo huo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho la TFF yakiendelea kufanyika kwa vilabu na mamlaka ya mpira.

Mwanachama huyo wa klabu ya Simba amesema kuruhusu matukio hayo yote kufanyika kwa pamoja,yatazuia wapenzi ambao ni wafuasi wa vilabu hivyo na pia ni viongozi katika chama cha CCM kushindwa kufuatilia mechi hiyo ambayo ina mvuto na inabeba tiketi ya ushiriki wa michuano ya kimataifa msimu ujao.

Pia ameongeza kuwa katika mchezo wa watani wa jadi uliopita,kuliendeshwa zoezi la uchangiaji wa damu na walioshiriki walizawadiwa fulana,lakini kwa sasa watagawa jezi ili kuongeza chachu kwa mashabiki wa vilabu vyote viwili.