Katibu Mkuu DAREVA Yusuph Mkarambati amesema walikuwa wakitarajia kupata wanafunzi 40 mpaka 50 lakini kutokana na changamoto mbalimbali wameweza kupata wanafunzi 16 kutoka vilabu mbalimbali vya mkoa wa Dar es salaam.
Mkarambati amesema, wahitimu wa kozi hiyo ya makocha watapelekwa shule za msingi na sekondari ambapo kuna uhaba wa walimu wa mchezo huo ili kuweza kupandisha viwango vya wanafunzi.
Mkarambati amesema, wanafunzi wanapoanza mapema michezo wanakuwa wazuri zaidi hapo baadaye ambapo watakuwa na uwezo wa kuutangaza mchezo kwa kutumia vipaji vyao.



