Lillard mwenye miaka 33 aliandika kwenye mtandao wake wa X zamani ukijulikana kama Twitter anasubiri kwa hamu kusubiri msimu mpya wa NBA kwa ajili ya kuitumikia timu yake mpya ya Milwaukee Bucks.
Damian Lillard alitangazwa kuwa miongoni mwa wachezaji 75 bora kuwahi kucheza ligi ya kikapu ya NBA mnamo mwaka 2021 huku msimu uliopita alikuwa na wastani wa kufunga alama 32.2 kwa mchezo mmoja na sasa anaungana na MVP mara mbili wa NBA Mgiriki Giannis Antetokounmpo ndani ya Bucks.