Jumapili , 29th Mei , 2022

Klabu ya Coastal Union ya Tanga imefuzu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup, baada ya kuifunga Azam FC kwa mikwaju ya penati 6-5 kwenye mchezo wa nusu fainali. Mchezo Uliochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Azam FC yafungwa na Coastal Union penati 6-5

Mchezo huu wa nusu fainali ya pili umechezwa dakika 120, baada ya dakika 90 kumalizika timu zikiwa zimetoshana nguvu kwa suluhu (0-0) hivyo mwamuzi Ramadhani Kayoko akaongeza dakika 30 za ziada nazo zikamalizka bila kupata mbabe hivyo mikwaju ya penati ikachukua nafasi.

Katika changamoto ya kupiga penati kila timu imepiga penati 7 Aazam FC wamekosa penati 2 na Coastal Union wamekosa penati moja na Coastal kuibuka na ushindi wa penati 6-5.

Katika hatua ya fainali coastal watacheza dhidi ya timu ya wananchi Yanga SC ambao wamewatoa Simba kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza kwa ushindi wa bao 1-0. Mchezo wa fainali unachezwa Julai 2, 2022. Jijini Arusha uwanja wa Sheikh Amri Abeid.