Jumatano , 7th Feb , 2024

Timu ya kikapu NBA yenye nyota wenye tuzo za U-MVP tatu laclippers ipo kwenye nafasi ya juu katika timu zinazopewa nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kutokana na matokeo yao ndani ya miezi miwili mfululizo.

Clippers ilimuongeza MVP wa msimu wa 2017-18 James Harden Novemba 01, 2023 na tayari walikuwa na MVP wa 2016-17 Russell Westbrook, MVP wa fainali mbili 2014 na 2019 Kawhi Leonard ambao kwasasa wapo kwenye ubora wa hali ya juu pamoja na nyota Paul George.