Jumatano , 22nd Jun , 2016

Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Obrey Chirwa ameelekea nchini Uturuki usiku wa jana kuungana na kikosi cha Yanga kilichoweka kambi nchini Uturuki.

Obrey Chirwa kulia akiwa na Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro uwanja wa Ndege jijini Dar es salaam

Chirwa raia wa Zambia aliyejiunga na Yanga akitokea FC Platinums ya Zimbabwe anatarajia kuanza mara moja mazoezi baada ya kutua nchini humo ili kuchukua nafasi ya Amis Tambwe.

Chirwa anatarajiwa kuchukua nafasi ya Tambwe katika mechi dhidi ya TP Mazembe kwa kuwa mshambuliaji huyo raia wa Burundi ana kadi mbili za njano zitazomzuia kucheza mechi hiyo.

Chirwa alirudi nchini akitokea Algeria alipokuwa na timu mara baada ya mchezo dhidi ya Mo Bejaia kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usajili wake.

Yanga itashuka dhidi ya TP Mazembe Juni 28 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni mchezo wake wa pili w ahatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika.