Ijumaa , 12th Oct , 2018

Mcheza tenisi namba 5 duniani, Alexander Zverev (21), raia wa Ujerumani, ameungana na nguli wa mchezo huo duniani, Rafael Nadal, Novak Djokovic, Roger Federer na Juan Martin del Potro, kama wachezaji ambao wamefuzu michuano ya tenisi ya kufunga msimu maarufu kama  'ATP Finals'

Kushoto ni Roger Federer, Alexander Zverev na Rafael Nadal.

itakayofanyika jijini London.

Zverev amepata nafasi hiyo baada ya kufuzu nusu fainali ya michuano ya Shanghai Masters, kwa kumtupa nje mchezaji namba moja wa Uingereza Kyle  Edmund kwa seti 6-4 6-4  kwenye robo fainali iliyopigwa mapema leo.

Ushindi huo wa Zverev umemuacha Edmund katika nafasi ya 12 kwenye kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za ATP ambazo zitafanyika nyumbani kwao kwenye dimba la 02 Arena. Edmund yupo nyuma kwa alama 1,590 dhidi ya Dominic Thiem ambaye anashika nafasi ya 8 hivyo ana kazi ngumu ya kufanya ili akate tiketi ya kucheza ATP.

Fainali za ATP hukutanisha nyota 8 wa tenisi duniani ambao huwania taji la mwisho la msimu wa tenisi. 

Zverev yeye sasa atakutana na nguli Novak Djokovic katika nusu fainali ya Shanghai Mastars baada ya Mserbia huyo kumshinda Kevin Anderson wa Afrika Kusini kwenye robo fainali kwa seti 7-6 (7-1) 6-3.