Jumapili , 4th Jul , 2021

Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia na Cape Town City ya Afrika Kusini, Charles Zulu, amefuzu vipimo kujiunga rasmi na timu ya Azam Fc.

Picha ya Mchezaji Charles Zulu na CEO wa Azam Fc

Klabu ya Azam imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao wa 2021/22 wa ligi kuu soka Tanzania bara na leo wamemtangaza kiungo huyo

"Tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumefanikiwa kunasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Charles Zulu, kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Cape Town City ya Afrika Kusini''.

''Tumemsajili baada ya kufikia makubaliano na Cape Town City, aliyokuwa akiichezea''.

''Zulu ambaye wakala wake ni Nir Karin, ataanza kuitumikia Azam FC msimu ujao 2021/22, ambapo kabla ya kutua Afrika Kusini alikuwa akikipiga kwa vigogo wa Zambia, Zanaco FC".

Picha Charles Zulu akifanyiwa vipimo