
Kiungo wa Yanga, Carlinhos akijiandaa kupiga mpira wa kona katika moja ya mchezo wa VPL.
Akizungumzia juu ya maendeleo ya kikosi chake, Kocha Cedric Kaze amesema Carlinhos anaumwa hivyo hatokua miongoni mwa wachezaji watakaocheza katika mchezo huo wa siku ya Alhamisi.
''Kikosi kipo vizuri, lakini tutawakosa wachezaji wanne ambao hawapo timamu kiafya, akiwemo kijana aliyepandishwa Fahad ana Malaria, Balama mapinduzi majeruhi wa muda mrefu, Abdul-Ahziz Makame ameanza mazoezi mepesi na Carlinhos anaumwa,lakini wengine waliosalia wapo vizuri''alisema Kaze.
Carlinhos amekua na msaada mkubwa wa mabao ya Yanga ambapo katika mechi nne, amefunga bao moja na pasi mbili za mabao katika msimu huu wa ligi kuu wa Tanzania bara.
Mchezo dhidi ya Polisi Tanzania utakua wa kwanza kwa kocha Cedric Kaze kuiongoza Yanga katika mashindano, na hii ni baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili ya kukinoa kikosi hicho akitwaa mikoba iliyoachwa na Zlatko Krmpotic aliyefutwa kazi baada ya siku 37 tu alizodumu mitaa ya Twiga na Jangwani.