Alhamisi , 28th Jan , 2016

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anatarajia kurejea uwanjani Jumatatu ijayo na kufanya mazoezi pamoja na wenzake.

Daktari wa Yanga Nassor Matuzya amesema, hali ya Cannavaro inaimarika na kama hali yake itaendelea kuwa nzuri wana matumaini makubwa kuwa ataungana na wenzake wiki ijayo.

Cannavaro amekuwa majeruhi kwa takribani miezi miwili sasa baada ya kuumia wakati akiitumikia timu ya taifa, Taifa Stars ambapo kwa sasa ameishaanza mazoezi mepesi pamoja na kufanya mazoezi ya gym pamoja na kukimbia taratibu.